KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Julai 9.

Muhtasari

•Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kericho, Busia, Nyeri, Kiambu, na Mombasa.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Julai 9. 

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kericho, Busia, Nyeri, Kiambu, na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mitaa ya Thigiri na Karen zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Chemosit na Litein katika kaunti ya Kericho zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Amerikwai na Malaba katika kaunti ya Busia pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kaiguri Gondo, Muthinga na Karima katika kaunti ya Nyeri litashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kiambu, sehemu za maeneo ya Gretsa, na mtaa wa Phase 13 zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Bombululu na Kisauni katika kaunti ya Mombasa pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.