Ujumbe umefika! Raila awaambia Gen Z kuhusu hendisheki

Kumekuwa na kizaazaa miongoni mwa vijana wa Kenya kuhusu wito wa Raila wa mazungumzo ya kitaifa, siku ya Jumanne.

Muhtasari
  • Katika chapisho kwenye X, Raila alionekana kwenye picha akiwa na Maseneta Edwin Sifuna (Nairobi), Eddy Oketch (Migori) na Crystal Asige (aliyeteuliwa) miongoni mwa wengine.
Image: RAILA ODINGA/ X

Kiongozi wa Azimio Raila Odinga sasa anasema kuwa amepokea jumbe kutoka kwa Wakenya kupinga mpango wowote wa hendisheki na Rais William Ruto.

Katika chapisho kwenye X, Raila alionekana kwenye picha akiwa na Maseneta Edwin Sifuna (Nairobi), Eddy Oketch (Migori) na Crystal Asige (aliyeteuliwa) miongoni mwa wengine.

"Nimeambiwa na viongozi kwamba mumesema hamtaki handshake. Ujumbe umefika," Raila alisema kwenye nukuu ya picha hizo.

Kumekuwa na kizaazaa miongoni mwa vijana wa Kenya kuhusu wito wa Raila wa mazungumzo ya kitaifa, siku ya Jumanne.

Katika tangazo, Rais Ruto na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila walikubaliana kuanza kongamano la siku sita la sekta mbalimbali.

Kongamano hilo, linalotarajiwa kuanza Jumatatu, Julai 15 na kuhitimishwa Jumamosi, litakuza mazungumzo ya kitaifa na kutafuta suluhu la kudumu kwa masuala muhimu ya Kenya.

Ruto alisisitiza umuhimu wa kongamano hilo akieleza kuwa litapendekeza njia ya kusonga mbele kwa nchi.

"Kongamano hili litaanza Jumatatu, wiki ijayo na kukamilika Jumamosi wiki ijayo, litakuwa la siku 6 na litapendekeza njia ya kuelekea nchi," Ruto alisema.

Kiongozi huyo wa ODM alikariri umuhimu wa kongamano hilo akisema litawapa Wakenya fursa ya kusikilizwa.