Rais William Ruto atahutubia taifa leo saa kumi jioni katika Ikulu ya Nairobi.
Hotuba hiyo inakuja baada ya wiki moja ya kufanya mabadiliko makubwa katika utawala wake ambayo yalisababisha kuvunjwa kwa baraza la mawaziri .
Pia hotuba hio inajiri wakati Wakenya wanatarajia mabadiliko zaidi katika utawala wake kulingana na wasiwasi uliotolewa na Gen Zs.
Rais William Ruto alivunja Baraza lake la Mawaziri na kuwarudisha nyumbani mawaziri wote na mwanasheria mkuu.
Uamuzi huo hauathiri Waziri Mkuu Musalia Mudavadi.
"Nimeamua kuwafuta kazi mara moja mawaziri na mwanasheria mkuu wa Baraza la Mawaziri la Kenya isipokuwa waziri mwenye mamlaka makuu na Katibu wa Baraza la Mawaziri," Ruto alisema.