Gavana Wavinya amshauri rais Ruto kuhusu uteuzi wa mawaziri wapya

Rais William Ruto aliwateua mawaziri 11 wa baraza la mawaziri kwa serikali yake mnamo julai 19.

Muhtasari

•Wavinya Ndeti amemshuri rais Ruto kuchukua muda wake ili kubaini mawaziri wapya watakaounda baraza lake la pili la mawaziri.

•Taifa  bado linasubiri rais  Ruto kutaja mawaziri zaidi wa baraza lake la pili la mawaziri.

GAVANA WA KAUNTI YA MACHAKOS WAVINYA NDETI
Image: KWA HISANI

Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti amemshauri Rais William Ruto kuchukua muda wake kutathmini na kuchagua watu watakaounda baraza lake la pili la mawaziri.

Akizungumza alipokuwa akihudhuria misa ya Jumapili  katika eneo la Athi river, Wavinya aliambia Rais kuwa wakenya wapo makini  jinsi atakavyoteua  baraza la mawaziri waliosalia.

Achukue muda, asikurupuke. Anapaswa kuchukua muda kusikiliza Wananchi, na kuchagua watu wanaowataka. Wanaoweza kutumikia wananchi,”  Wavinya alisema.

Gavana huyo alidai kuwa  ingawa wafanyikazi wa umma hawakosi  makosa, Rais ana fursa ya kuwatambua na kuwachagua watu ambao wanaweza kuwafanyia kazi wakenya.

Rais William Ruto aliwateua mawaziri 11 wa baraza la mawaziri kwa serikali yake julai 19. Uteuzi huo ulijiri wiki kadhaa baada ya rais kulifuta baraza lake lote la mawaziri isipokuwa waziri mkuu Musalia Mudavadi.

Taifa  bado linasubiri rais  Ruto kutaja mawaziri zaidi wa baraza lake la pili la mawaziri.