KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Julai 24.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti kumi za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Bomet, Nyeri, Tharaka Nithi, Trans Nzoia, Kakamega, Kisii, Migori, Meru, Kiambu, na Kwale.
Katika kaunti ya Bomet, maeneo ya Kapkwen na Makimeny yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Kairuthi na Gathumbi katika kaunti ya Nyeri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kaareni na Kambururu katika kaunti ya Tharaka Nithi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Katika kaunti ya Trans Nzoia, sehemu kadhaa za maeneo ya Natwana na Moisbridge zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.
Eneo la Lubao Shikusa katika kaunti ya Kakamega litakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Kamagambo katika kaunti ya Kisii litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Oyani Masai na Ulanda katika kaunti ya Migori yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Katika kaunti ya Meru, sehemu za maeneo ya Gitoro, Kiirua na Kibirichia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Wakati huohuo, sehemu ya eneo la Ngoigwa katika kaunti ya Kiambu pia zitaathirika.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Msambweni na Shimoni katika kaunti ya Kwale pia zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.