Masengeli, Lagat Waapishwa kuwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (Picha)

Waliapishwa, katika hafla fupi iliyofanyika katika mahakama ya juu iliyoongozwa na CJ Koome.

Muhtasari

•Jukumu la DIG-KPS linahusisha kuamuru, kudhibiti, na kusimamia huduma ya polisi ya Kenya chini ya uongozi wa IG.

• DIG-APS ana jukumu la kuongoza huduma ya polisi ya utawala na anafanya kazi chini ya maelekezo na udhibiti wa IG.

Jaji Mkuu Martha Koome akiwa na Eliud Lagat na Gilbert Masengeli wakati wa kuapishwa kwao katika mahakama ya juu mnamo Julai 25, 2024.
Jaji Mkuu Martha Koome akiwa na Eliud Lagat na Gilbert Masengeli wakati wa kuapishwa kwao katika mahakama ya juu mnamo Julai 25, 2024.
Image: Hisani

Naibu inspekta jenerali wa polisi (DIG-KPS)  Eliud Lagat na naibu inspekta jenerali wa polisi wa utawala (DIG-APS) ,Gilbert Masengeli waliapishwa Alhamisi.

Waliapishwa, katika hafla fupi iliyofanyika katika mahakama ya juu na kuongozwa na Jaji mkuu na rais wa mahakama ya juu ya Kenya Martha Koome.

DIG-APS Gilbert Masengeli akula kiapo Julai 25,2024
DIG-APS Gilbert Masengeli akula kiapo Julai 25,2024
Image: Hisani

Inspekta Jenerali Douglas Kanja Kirocho baada ya hapo alikabidhi Kamandi ya NPS kwa Masengeli. DIG Masengeli sasa atakuwa kaimu inspekta jenerali wa jeshi la polisi nchini.

Hii inafuatia uteuzi wa Kanja kama inspekta jenerali wa polisi mnamo Juni 25, 2024, na Rais William Ruto.

Eliud Lagat ,aapishwa Julai 25,2024
Eliud Lagat ,aapishwa Julai 25,2024
Image: hisani

Jukumu la DIG-KPS linahusisha kuamuru, kudhibiti, na kusimamia huduma ya polisi ya Kenya chini ya uongozi wa inspekta jenerali.

DIG-APS ina jukumu la kuongoza huduma ya polisi ya utawala na inafanya kazi chini ya maelekezo na udhibiti wa inspekta polisi.