Tazama kaunti 7 zitakazoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumanne

Maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni

Muhtasari

•KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Mombasa, Kajiado, Kisumu, Nyeri,Homa Bay na Bungoma.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Agosti 13. 

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Mombasa, Kajiado, Kisumu, Nyeri,Homa Bay na Bungoma.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kibiku Feeder, Ruai Sewage, Joska Feeder, Utawala, Njiru, Vicken Feeder, North Impact, KCC Village, Bomas of Kenya na Galleria zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Kitengela na Isinya katika kaunti ya Kajiado zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Sondu, Nyabondo, na Sigoti katika kaunti ya Kisumu yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Maeneo ya Khachonge, Bwake, na Luuya Girls katika kaunti ya Bungoma yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Katika kaunti ya Nyeri, maeneo ya Amboni Dairy, Laini Saba, PCEA Amboni, Wendiga, na Kiguru yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Ogandi Girls, Ndiru, na Arujo katika kaunti ya Homa Bay yataathirika kati ya saa tatu na saa kumi alasiri.

Eneo la Mshomoroni katika kaunti ya Mombasa pia litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.