Rais Ruto awatunuku wanariadha walioshinda dhahabu kwenye Olimpiki Ksh 3M kila mmoja

Mwanaridha Beatrice Chebet alishinda dhahabu mbili huku Faith Kipyegon na Emmanuel Wanyonyi wakijishindia dhahabu moja kila mmoja.

Muhtasari

• Mwanaridha Beatrice Chebet alishinda dhahabu mbili huku Faith Kipyegon na Emmanuel Wanyonyi wakijishindia dhahabu moja kila mmoja.

• Kenya ilimaliza katika nafasi ya kwanza barani Afrika kwa msimamo wa medali na nafasi ya 17 kote duniani.

RUTO AKIMZAWADI FAITH KIPYEGON.
RUTO AKIMZAWADI FAITH KIPYEGON.
Image: FACEBOOK//WILLIAM RUTO

Rais William Ruto amewakaribisha rasmi wanariadha wa Kenya waliowakilisha taifa katika mashindano ya Olimpiki za jijini Paris Ufaransa.

Wanariadha hao walirejea nchini Usiku wa Jumanne baada ya mwezi mzima nchini Ufaransa ambako walipeperushwa kwa fahari bendera ya taifa katika mashindano hayo makubwa ya spoti yanayofanyika kila baada ya miaka minne.

Ruto, ambaye aliongozana na viongozi wengine serikalini kaitka mji wa Eldoret aliwakaribisha na kuwatunuku washindi wa medali za dhahabu shilingi milioni 3 kila mmoja.

Kenya ilijishindia jumla ya medali 11, 4 kati yao zikiwa za dhahabu.

“Fahari ya Kenya katika riadha haiishii katika medali 11 ambazo tulishinda katika Michezo ya Olimpiki. Uwezo wetu unabaki kuwa mkubwa na haujatumiwa. Tutaongeza ushirikiano na wadau ili kuinua wasifu wetu kama Nchi ya Mabingwa. 

RUTO AKIMZAWADI BEATRICE CHEBET
RUTO AKIMZAWADI BEATRICE CHEBET

Tuliwakaribisha na kuwatambua nyota wetu wa dhahabu katika State Lodge, Eldoret, baada ya kuibuka na ushindi katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024. Hongera Timu ya Kenya,” Rais Ruto alichapisha kwenye picha hizo akiwakabidhi hundi.

Mwanaridha Beatrice Chebet alishinda dhahabu mbili huku Faith Kipyegon na Emmanuel Wanyonyi wakijishindia dhahabu moja kila mmoja.

RUTO AKIMZAWADI EMMANUEL WANYONYI
RUTO AKIMZAWADI EMMANUEL WANYONYI

Igahamike kwamba Chebet alipokea jumla ya shilingi milioni 6 kutokana na dhahabu zake mbili.

Kenya ilimaliza katika nafasi ya kwanza barani Afrika kwa msimamo wa medali na nafasi ya 17 kote duniani.

Rais Ruto yuko mjini Eldoret katika hafla ya kupandishwa kwa hadhi ya mji huo kuwa jiji.