KPLC yatangaza maeneo yatakayokosa umeme leo, Jumanne

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Agosti 20.

Muhtasari

•KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Bungoma, Nyeri, Kakamega, na Taita Taveta.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumanne, Agosti 20. 

Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Bungoma, Nyeri, Kakamega, na Taita Taveta.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Kitsuru zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la West Kenya Sugar Factory Naitiri katika kaunti ya Bungoma litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Musaga na Samisi Market katika kaunti ya Kakamega yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Nyeri, maeneo ya Ihithe na Hubuini yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Msumarini, Kurawa na Tarassa katika kaunti ya Taita Taveta pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.