Marco Joseph: Msanii wa kundi la Zabron Singers ameaga dunia

Waimbaji hao ni zaidi ya kikundi cha muziki, wao ni familia. Wengi wao wanatoka katika familia moja, wakati wengine ni marafiki wa karibu wa familia.

Muhtasari

• Marco Joseph Bukulu ni mmoja wa Zabron Singer's 

• Aliaga dunia jana usiku akipokea matibabu katika  hospitali ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), jijini Dar es salaam.

MSANII WA ZABRON SINGERS.
MSANII WA ZABRON SINGERS.
Image: HISANI

Marco Joseph Bukulu, mmoja wa kundi la wasanii wa injili la Zabron Singer's ameaga dunia.

Joseph aliaga dunia jana usiku akipokea matibabu ya ugonjwa wa moyo katika hospitali ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) ,jijini Dar es Salaam.

Kulingana na Mzee Zabron, kifo cha Joseph kilisababishwa na mshtuko wa moyo wa ghafla lililoanza Jumapili iliyopita.

Joseph ameaga dunia akiwa kwa miaka yake ya 40. Alijulikana sana na kikundi chake cha Zabron Singer's ambao wanajulikana kwa nyimbo nyingi kama ' Sweetie sweetie', 'Mkono wake Bwana', 'Uko Single' na zingine nyingi.

Zabron Singer's ni kikundi cha muziki wa kidini kutoka Tanzania kinachobobea katika muziki wa Kikristo.

Waimbaji hao ni zaidi ya kikundi cha muziki, wao ni familia. Wengi wao wanatoka katika familia moja, wakati wengine ni marafiki wa karibu wa familia.

 Mwenyekiti Obeid Kazimili alionyesha huzuni yake kupitia chapisho kwenye Facebook akisema "Mwenyekiti wa Zabron Singers ninasikitika kutangaza kifo cha mwimbaji mwenzetu ndugu Marco Joseph Bukulu ambaye alikuwa makamu mwenyekiti na msaidizi wa Zabron Singers kilichotokea usiku wa leo huko jijini Dar es salaam katika hospitali ya Jakaya. Taarifa zaidi tutazitoa hapo baadaye za taratibu za maziko. Bwana awabariki"