•KPLC imesema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Meru, Laikipia, na Nyeri.
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Agosti 22.
Katika taarifa ya Jumatano, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Meru, Laikipia, na Nyeri.
Katika kaunti ya Meru, sehemu za maeneo ya Mikinduri na Kigucwa zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Makutano na Kongoni katika kaunti ya Laikipia yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Wakazi wa mji wa Othaya na Mahiga katika kaunti ya Nyeri pia watashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.