•Maandamano hiyo ambayo yamelemaza shughuli za masomo katika shule za upili kote nchini.
•Kuppet imekuwa ikiwashauri wazazi kusalia na wanao nyumbani hadi pale wataafikiana na TSC kurejea kazini.
Chama cha walimu KUPPET bado kinagoma licha ya amri ya mahakama kusitisha mgomo huo.
Maandamano hiyo ambayo yamelemaza shughuli za masomo katika shule za upili kote nchini yalitokana na hatua ya TSC kutotekeleza mkataba wa makubaliano kati yao na walimu.
Wanachama wa KUPPET tawi la Uasin Gishu walivamia shule ya upili ya Uasin Gishu baada ya kufahamishwa kuwa kuna walimu wanafundisha licha ya wao kugoma. Licha ya mlinzi kufunga lango, kuna walimu ambao walipanda ukuta na kuingia ndani ya shule na kufungulia wenzao ambao walikuwa nje.
Kwenye video walimu hao walisikika wakiimba "Waasaliti!Wasaliti!Wasaliti!" wakiwa ndani ya shule wakitafuta wenzao ambao walikuwa tayari washatoroka.
Kulingana na mwenyekiti wa Kuppet tawi la Uasin Gishu Sosthen Bellat walienda kutoa walimu lakini hawakuwapata kwani walikuwa washatoroka. Pia alisisitiza kuwa wataendelea na mgomo.
"Sisi tunaendelea na mgomo leo, kesho, kesho kutwa, next week, next month, next year......Tumekuja tumetoa walimu hapa, wametoroka hatujawapata...Hatuwezi kung'ang'ana kuwatafutia pesa na kuna watu wanaendelea kufunza...Wazazi wakae na watoto wao" Sosthen alisema.
Maandamano hayo yataendelea mpaka matakwa ya walimu yatakaposhughulikiwa.
Kuppet imekuwa ikiwashauri wazazi kusalia na wanao nyumbani hadi pale wataafikiana na TSC kurejea kazini.