Ruto: Sina jina la mtu hata mmoja aliyeripotiwa kutekwa nyara au kupotea wakati wa maandamano

“Kama kuna familia yoyote ambao mpendwa wao alikwenda katika maandamano na hakurejea nyumbani, ningependa kujua majina yao kwa sababu nitachukua hatua kali, kwa sababu vile ninaongea na nyinyi leo, sina hata jina moja la mtu aliyetekwa nyara au kupotea,” aliongeza

Muhtasari

• “Kama uko na jina la mtu alienda maandamano akapotea, familia yake wakuje wampe PS Omollo majina na tutashughulikia suala hilo kwa sababu Wakenya wana haki ya kujieleza," rais alisema.

RUTO,
RUTO,
Image: FACEBOOK

Rais William Ruto kwa mara nyingine amesisitiza kwamba mpaka sasa, hajapatiwa jina la mtu hata mmoja aliyeripotiwa kutekwa nyara au kupotea kwa njia zisizoeleweka wakati wa maandamano ya Gen Z.

Akizungumza na wakaazi wa Kisumu usiku wa Alhamisi, rais Ruto alisisitiza kwamba katika utawala wake, amehakikisha na atazidi kuhakikisha kwamba hakuna Mkenya atakayetoweka na mwili wake kupatikana Mto Yala au katika mto wowote ule akiwa ameuawa.

“Nilitoa hakikisho kwa watu wav Kenya na ninataka kuwatazama usoni na niwaambie kwamba katika uongozi wangu, sitaku hali kutokea kwamba Mkenya anatoweka. Kulikuwa na siku miili 20-30 ilikuwa inapatikanav Mto Yala wakiwa wameuawa, ningependa kuwaahidi kwamba chini ya uongozi wangu hakuna Mkenya atakayepatikana ameuawa katika sehemu yoyote,” alisisitza.

Ruto aliwataka watu wa Kisumu ambao walipoteza wapendwa wao kwa njia zisizoeleweka wakati wa maandamano kutoa majina yao kwa katibu katikac wizara ya usalama wa ndani, Raymond Omollo ili suala lao kushughulikiwa.

“Kama kuna familia yoyote ambao mpendwa wao alikwenda katika maandamano na hakurejea nyumbani, ningependa kujua majina yao kwa sababu nitachukua hatua kali, kwa sababu vile ninaongea na nyinyi leo, sina hata jina moja la mtu aliyetekwa nyara au kupotea,” aliongeza.

“Kama uko na jina la mtu alienda maandamano akapotea, familia yake wakuje wampe PS Omollo majina na tutashughulikia suala hilo kwa sababu Wakenya wana haki ya kujieleza katika viwango vya kisheria, kwa sababu hakuna Mkenya anastahili kutendewa unyama kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa,” aliongeza.