• Katika kikao hicho, wananchi walipata nafasi adimu ya kumuuliza Rais Ruto maswali na kupata majibu yao.
• Mmoja alimuuliza rais kuhusu suala la baadhi ya viongozi katika serikali kudai kwamba wao ndio wenye hisa katika setrikali.
Rais William Ruto usiku wa Alhamisi alikuwa na kikao na wakaazi wa jiji la Kisumu wakati anaendelea na ziara yake ya siku 4 katika uliokuwa mkoa wa Nyanza.
Katika kikao hicho, wananchi walipata nafasi adimu ya kumuuliza Rais Ruto maswali na kupata majibu yao.
Mmoja alimuuliza rais kuhusu suala la baadhi ya viongozi katika serikali kudai kwamba wao ndio wenye hisa katika setrikali.
Akijibu swali hilo, Ruto alisisitiza kwamba kila mwananchi wa Kenya ana mgao wake wa hisa na hivyo makubaliano ni kwamba Kenya ni ya kila mtu bali si ya wananchi walio karibu na uongozi.
“Tulikubaliana kwamba sisi wote ni shareholders wa nchi hii, kila mmoja wetu. Kila Mkenya ana haki, kila mlipa ushuru ana haki, hivyo ningependa kuwahakikishia kwamba tumekubaliana ni sharti tuondoe siasa za kikabila, siasa za kujitenga, siasa za kuleta mgawanyingo kati yetu, na hiyo ndio sababu nilichukua fursa ya mapema kabisa kuanzisha serikali pana,” kiongozi wa taifa alisema.
Kauli ya kuwa baadhi ya wananchi ndio wenye hisa katika serikali ya Kenya Kwanza ilibuniwa na naibu rais Rigathi Gachagua ambaye alidai kwamba waliopigia serikali kura ndio wanafaa kupewa kipaumbele katika miradi ya maendeleo.