•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Septemba 2.
Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi, Kisumu na Homabay.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Westlands na Lower Kabete zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za eneo la Kibos katika kaunti ya Kisumu zitaathirika kati ya saa mbili unusu na saa tisa alasiri.
Maeneo ya Adiedo na Omboga katika kaunti ya Homabay pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.