“Tumewaacha wanafunzi wafunzwe na ulimwengu,” walimu wanaogoma waimba (video)

“Tumeacha, tumeacha, tumeacha shule zote tumeacha, tumeacha wafunzwe na ulimwengu,” waliimba kiitikio hicho.

Muhtasari

• “Tumeacha, tumeacha, tumeacha shule zote tumeacha, tumeacha wafunzwe na ulimwengu,” waliimba kiitikio hicho.

KUPPET wakiwa mgomo
KUPPET wakiwa mgomo
Image: KUPPET//Facebook

Chama cha walimu wa shule za upili na vyuo anuwai, KUPPET wameapa kuendelea na mgomo wao unaoingia katika wiki ya pili sasa.

Wakiongozwa na katibu mkuu Akelo Misori, walimu hao waliapa kuendelea na mgomo wao hadi pale serikali itakapowapa sikio la usikivu na kutatuac maswala yao.

Walimu haop walikwenda hatua zaidi na kutunga wimbo wakisema wameamua kuondoka darasani na kuwaacha wanafunzi mikononi mwa ulimwengu ili uwafunze.

“Tumeacha, tumeacha, tumeacha shule zote tumeacha, tumeacha wafunzwe na ulimwengu,” waliimba kiitikio hicho.

Wiki moja baada ya mgomo kuanza, Baraza la Kitaifa la Uongozi la KUPPET lilikutana jijini Nairobi kukagua maendeleo ya hatua yao ya kiviwanda. Azimio lao bado halijabadilika: mgomo utaendelea hadi matakwa yao yatimizwe.

Muungano huo umeguswa hasa na athari za mgomo huo katika maandalizi ya watahiniwa wa kidato cha nne wanaotazamiwa kufanya mitihani yao mwishoni mwa muhula huu.

Hapo awali mgomo huo uliitishwa ili kushinikiza kutekelezwa kwa Mkataba wa Mapatano ya Pamoja wa 2021-2025 (CBA).

Huku serikali ikichukua hatua ya kutekeleza awamu ya pili ya CBA, KUPPET inashikilia kuwa nyongeza ya mishahara haitoshi kukidhi mahitaji ya walimu.