•Mwanariadha Rebecca Cheptegei,ameaga dunia kutoka na majeraha ya kuteketezwa na petroli na mpenziwe wa Kenya Dickson Ndiema.
•Rebecca amefariki licha ya wizara ya Michezo kusema itagharamikia matibabu spesheli Nairobi.
•Kisa hicho cha ukatili kilitokea katika kaonti ya Trans Nzoia baada ya mpenziwe kutoka kanisani kama inavosemekana.
Mwanariadha kutoka taifa la Uganda na ambaye aliteketezwa kiwango cha asilimia 80 na mpenziwe kutoka Kenya,Dickson Ndiema amefariki hii leo .Kulingana na taarifa zinashiria kwamba,Rebecca,alikuwa anazidi kupata matibabu.
Kitendo hiki cha kinyama kilitendeka katika kaonti ya Trans Nzoia,huku mwanariadha huyo akipata majeruhi ya kuchomeka mwili wake kiwango cha juu cha aslimia 80,na kuweka maisha yake hatarini licha ya kupelekwa hosipitalini.
Kifo chake kinajiri masaa machache baada ya wizara ya michezo hapa Kenya, kuahidi kuwa watashughulikia matibabu ya kispesheli hapa Kenya siku ya leo.
Ndiema,anasemekana kuwa alikuwa ametoka kanisani baada ya kumumwagilia petroli na kisha kumteketeza Rebecca.
Licha ya kukimbizwa hosipitali ya Moi Teaching Referral Hospital,majeraha aliyokuwa nayo yaliashiria hatari kubwa kwa maisha yake.