•Katika taarifa ya Jumatano, KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nakuru, Uasin Gishu, Elgeyo Marakwet, Meru, Murang'a na Kiambu.
KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Septemba 5.
Katika taarifa ya Jumatano, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nakuru, Uasin Gishu, Elgeyo Marakwet, Meru, Murang'a na Kiambu.
Katika kaunti ya Nakuru, maeneo ya Olrongai, Tulwobmoi, Pipeline, na Wanyama yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Sosioni na Chemaluk katika kaunti ya Uasin Gishu yataathirika kati ya saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Chebororwa katika kaunti ya Elgeyo Marakwet litaathirika kati ya saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Mafuko na Runogone katika kaunti ya Meru zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Murang'a, maeneo ya Gatura na Kiarutara yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Mji wa Juja, Chuo Kikuu cha JKUAT, Kirigiti, Gichocho, Kiambu High, mji wa Limuru, na sehemu za Lironi katika kaunti ya Kiambu pia kutaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.