KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Ijumaa

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Septemba 6.

Muhtasari

•Katika taarifa ya Alhamisi, KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nairobi, Kakamega, Homabay, na Kisii.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Septemba 6. 

Katika taarifa ya Alhamisi, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nairobi, Kakamega, Homabay, na Kisii.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Kilimani zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za eneo la Khwisero katika kaunti ya Kakamega zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Gendia, Kosele, na Namba katika kaunti ya Homabay yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Wakati huohuo, sehemu za maeneo ya Suneka, Gesonso na Iterio katika kaunti ya Kisii pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.