Morara Kebaso aeleza sababu ya kutoroka eneo la tukio baada ya gari lake kuhusika katika ajali

“Nina maadui wengi sana kuanza kubahatisha ni nani anayeweza kuifanya. Viongozi wa serikali ambao tumewafichua, upinzani unaohisi tunachukua nafasi zao..." alisema.

KEBASO.
KEBASO.
Image: FACEBOOK

Mwanaharakati wa kutoa elimu ya kiraia nchini, Morara Kebaso Snr amevunja kimya chake, saa chache baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani.

Morara Kebaso alikuwa katika harakati za kutoa elimu ya kiraia katika kaunti ya Embu ambapo wakati wa kurejea Nairobi, gari lake lilihusika katika ajali baada ya kugongwa na gari jingine.

Kebaso amevunja kimya chake na kusema kwamba hakuweza kuumia lakini alilazimika kutroka eneo la ajali kwa haraka akitumia gari jingine.

Akielezea sababu ya kufanya hivyo bila kuwangoja maafisa wa trafiki, Morara alisema kwamba alipata dhamira kwamba ana maadui wengi wanaomzungumza na wangeweza kutumia fursa ya ajali hiyo ndogo ili kumdhuru zaidi.

“Jana baada ya ajali nilitoweka kwa kasi sana eneo la tukio kwa gari lingine maana wakati mwingine ajali hutumika kuleta mkanganyiko ili jambo halisi litokee. Sitaki kulaumu mtu bila ushahidi lakini sasa najua nimehesabiwa muda.”

“Nina maadui wengi sana kuanza kubahatisha ni nani anayeweza kuifanya. Viongozi wa serikali ambao tumewafichua, upinzani unaohisi tunachukua nafasi zao, machifu wa makabila wanaoinuka wanaohisi ujumbe wetu unaweza kuwapunguzia ushawishi, wagombea urais wanaodhani nitashindana nao, wakandarasi waliolipwa pesa na kutoweka huruma ya mafisadi. Orodha haina mwisho,” alisema.

“Hakika nitahakiki maelezo yangu ya usalama kwenda juu. Na nitaepuka mikutano ambayo inamwagika hadi usiku. Ninashukuru kuwa hai. Na ninaamini ni kwa sababu lakini pia kwa msimu kwa sababu siku moja nitakufa,” aliongeza.