Khalwale afurahi baada ya bintiye kujizolea alama 402 katika mtihani wa KCPE

Muhtasari
  • Khalwale afurahi baada ya bintiye kujizolea alama 402 katika mtihani wa KCPE
Seneta wa zamani wa Kakamega Boni Khalwale
Seneta wa zamani wa Kakamega Boni Khalwale
Image: MAKTABA

Bintiye aliyekuwa Seneta wa Kaunti ya Kakamega Boni Khalwale alikuwa miongoni mwa watahiniwa 1,214,301 waliofanya mtihani wa KCPE wa 2021.

Saa chache baada ya kutangazwa rasmi kwa matokeo ya mtihani wa KCPE, Khalwale alienda kwenye Twitter na kusambaza ujumbe wa shukrani kufuatia utendakazi wa kuvutia wa bintiye.

"Familia yangu na mimi, kwa njia 1000 maalum tunamshukuru Mungu, walimu na wasio walimu wa Shule ya Msingi ya Malinya na Shule ya Kakamega Hill Junior kwa 402!" Khalwale aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Melissa Khamwenyi Khalalwe, bintiye Boni, alijizolea 402.

Kulingana na matokeo yaliyoshirikiwa na Khalwale, Melissa Khamwenyi Khalwale wa nambari 37615027005 alipata matokeo kama yafuatayo: "ENG 86-A, KIS 83-A, MAT- 83-A, SCI 66-B, SSR 84-A". Alama zote zinaongeza hadi alama 402.

Katika matokeo yaliyotolewa, mwanafunzi wa kwanza, Bruce Mackenzie alijizolea alama 428