Gladys Wanga amtafuta mwanamume aliyebusu picha yake kwenye bango

Muhtasari
  • Gladys Wanga amtafuta mwanamume aliyebusu picha yake kwenye bango
Image: GLADYS WANGA/TWITTER

Mwakilishi wa Wanawake wa Homabay Gladys Wanga anamtafuta mwanamume ambaye alionekana akibusu picha yake kwenye bango la kampeni.

Katika picha aliyoshiriki kwenye mitandao ya kijamii, mwanamume aliyekuwa ameshikilia sahani ya chakula alisimama kwenye bango la Gladys Wanga.

Kisha akainama kumbusu mdomo wake.

"Kuna mtu anayemfahamu kijana huyu? Tafadhali shiriki mawasiliano yake," Gladys Wanga alishiriki kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Ni picha ambayo imeibua hisia tofauti miongoni mwa wakenya na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

MAX: And the guy just made it.

Kijana ya GishagI: He is engaging in gender-based violence...

Juma G : Another "Githeri Man" moment... This can be called "The Chips Mwitu Man" moment... Gladys Wanga is so down to earth... No manifesto, no plan, but she will change that whatever county... Way to go!

Mash: That photo was souped up. Wanga doesn't look like this. The poor guy is kissing a fake!