Mbunge anaswa akitusi familia yenye ushawishi mkubwa nchini

Muhtasari

•Mbunge huyo ambaye amejawa na  wasiwasi kwa sasa anawasiliana na wale walio karibu na familia hiyo yenye nguvu

Shughuli katika bunge la kitaifa
Shughuli katika bunge la kitaifa
Image: MAKTABA

Mbunge mmoja yupo matatani baada ya mazungumzo yaliyovuja mtandaoni  kumuweka mwanasiasa huyo kwenye mzozo na familia muhimu kisiasa. Katika mazungumzo hayo, mbunge huyo anasikika akimsema vibaya mtu mmoja wa familia hiyo, jambo ambalo wapinzani wake wanalitumia sasa kujenga sintofahamu kati yake na familia hiyo yenye ushawishi mkubwa. Mbunge huyo ambaye amejawa na  wasiwasi kwa sasa anawasiliana na wale walio karibu na familia hiyo yenye nguvu. Anaendesha simulizi kwamba mazungumzo yaliyovuja, ambayo yanamfichua vibaya, yalikuwa ni yaliundwa na maadui wake wa kisiasa waliodhamiria kumtimua  bungeni.

***

Wabunge waliokuwa wakiztembea na gavana mgombea ugavana kutoka Magharibi mwa Kenya wamemwacha. Mwanasiasa huyo ameachwa ajiangalie  mwenyewe katika azma yake ya kuchukua wadhifa wa mkuu wa kaunti. Corridors inaambiwa kwamba mwanasiasa huyo pia angetaka kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho  baada ya kugundua kuwa wabunge hao walioondoka na wafuasi aliokuwa na. Imani miongoni mwa wapiga kura wake ni kwamba hakuwahi kusaidia wakati alipokuwa na wadhifa mkubwa nchini. Wapiga kura wamekuwa wakimpa mapokezi baridi mwanasiasa huyo katika vituo mbalimbali anavyopita, ikidaiwa kuwa ni baada ya wabunge kuwatia sumu akilini.

***

Mbunge anayetambulika  kutoka eneo la Magharibi mwa nchi ananunua kimyakimya alama na saini zinazofaa kwa ajili ya matumizi katika uchaguzi wa Agosti ikitokea chama chake hakitamkabidhi tikiti kama inavyodaiwa sana. Mbunge huyo ambaye anashuku kuwa mpinzani wake anazidi kuwa kipenzi cha mamlaka zilizopo anaweka kila kitu tayari kwa mabadiliko ya kuwa mgombeaji Huru. Mtu huyo anadai ametekeleza ahadi zake kwa wapiga kura na taaluma yake ya kisiasa haiwezi kukatizwa kwa sababu ya maslahi ya baadhi ya viongozi wakuu katika chama chake.

(Utafsiri: Samuel Maina)