Ala!Aliniacha baada ya kumnyima shilingi 50-Mwanamke asimulia sababu ya kuachwa na mumewe

Muhtasari
  • Sio siri kila mkenya amepitia maisha magumu hasa wakati janga la corona liliripotiwa nchini mwaka wa 2020
black-woman-crying-
black-woman-crying-

Ni furaha ya kila mwanamke au kila wanandoa kusaidiana katika ndoa hasa wakati huu maisha yamekuwa magumu kwa kila mkenya, haya ni matamshi ya Diana ambaye alisimulia sababu ya kuvunjika kwa ndoa yake ya miaka 3.

Sio siri kila mkenya amepitia maisha magumu hasa wakati janga la corona liliripotiwa nchini mwaka wa 2020.

Nilipokuwa kwenye  ziara zangu, huku nikitangamana na wakenya, nilipatana na Diana mwenye amekuwa akishika tama kwa miezi 3sasa baada ya kuachwa na mumewe

Lakini sababu kuu ya kuachwa na mumewe licha ya kubarikiwa na mtoto mmoja ni ipi?

Huu hapa usimulizi wake;

"Mume wangu aliponioa sijawahi muona amerauka kama wanaume wengine kuenda kutafuta anagalau kibarua ili tupate mkate wa kila siku, bora amsubiri amuite kazi ndogo ndogo ya mikono lakini sio aende kwenye kampuni kubisha au kutuma barua kutafuta kazi

Sababu kuu ya kuniacha ni kwa maana aliniomba shilingi hamsini, nilizokuwa nimeuza kwenye kijibanda changu kidogo nikamyima

Keshoye alikusanya virago vyake vyote na kuniacha,ni miezi 3 sasa na hajawahi kutujulia hali, bali sina haja naye kwani huyo ni mwanamume mvivu."