'Nilipata vest chini ya kitanda,'Mwanamume asimulia sababu ya kumuacha mkewe

Muhtasari
  • Kila ndoa ina changamoto na hamna ndoa mabyo ni kamili kulingana na wanandoa wengi
sad man
sad man

Ndoa karne hii ya sasa ni changamoto kwa wanadoa wengi kwani hawakubali kukabiliana na changamoto zake.

Kila ndoa ina changamoto na hamna ndoa mabyo ni kamili kulingana na wanandoa wengi.

Nikiwa kwenye ziara yangu nilipatana na mwanamume ambaye amekuwa mpweke kwa mwezi mmoja sasa.

KUlingana na Martin, aliachanana na mke wake baada yake kuwa na mipango ya kando na kuleta wanaume kwenye kitanda chao cha ndoa.

Mambo yalifika kilele baada ya Martin kutoka kazi, na kumpata mkewe akiwa na mwanamume ilhali hakumuona.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilitoka kazi mwezi jana nikmpata mke wangu na mwanamume, ilhai aliniambia ni binamu yake ambae alikuwa ametoka nyumbani

Siku moja baadaye nilipata 'vest na Boxer' chini ya kitanda, nilipomuuliza aliniambia kwamba amechoka na mimi na kwamba mimi nni maskini ilhali alikuwa anataka mwanamume ambaye ni tajiri na wala sio mlinzi kama mimi

Tulikuwa kwa ndoa kwa miaka 6 sasa, na tumebarikiwa na watoto 2, nilimuacha na nikaenda kukondisha nyumba kwingine kwani nimeskia nimechoka naye

Hata kunichapa alikuwa ananichapa, kweli wanaume wamekuwa wakipitia mengi kwenye ndoa na kuumia kimoyomoyo kwa sababu wanaogopa kukejeliwa."