Alinilazimisha nilale na mumewe la sivyo anifute kazi-Mwanamke asimulia masaibu haya

Muhtasari
  • Unyanyasaji wa kingono umeshuhudiwa sana nchini, huku asilimia kubwa ya wanawake wakinyanyaswa na kusalia kimya
sad woman
sad woman

Kama hujayaona na kuyaskia yote kuna baadhi yao ambao wameona yote na hata kukata tamaa ya kuishi.

Unyanyasaji wa kingono umeshuhudiwa sana nchini, huku asilimia kubwa ya wanawake wakinyanyaswa na kusalia kimya.

Kuna baadhi yao hunyanyaswa na waajiri wao, hasa vijakazi wengi hupitia maisha magumu endapo wamepata mwajiri mwenye tabia kama hiyo.

Licha ya changamoto zote wamekuwa wakiendelea na maisha yao, na hata kuzidi kufanya kazi kwenye vyumba vya waajiri hao, kwani hawana mapato mengine.

Huku nikiwa kwenye ziara yangu nilipata na Rose mwanamke ambaye ameona yote, na kukata tamaa ya kuishi.

Rose alinisimuia jinsi alivyokuwa msichana alinyanyaswa na mwajiri wake mwanamke.

Si hayo tu bali kulingana na Rosse mwajiri wake alikuwa ana mlazimisha afanye ngono na mume wake bila ya kujua sababu.

Huu hapa usimulizi wake;

"Kwetu hatukubarikiwa na pesa nyingi, ilinibidi niachie masomo yangu katikati ili niwee kumsaidia mama yangu ambaye aliuwa mjane, baba yangu aliaga dunia nikiwa darasa la sita, na kutuacha na mma yangu ambaye alikuwa na watoto 5

Baada ya kukamilisha masomo ya msingi,nilitafuta kazi ya nyumba, kwa kweli unyanyasaji wa kingono haujaanza hizi majuzi bali ulianza kitambo ni vile wanawake hatukuwa na uwezo wa kusema

Nilifanikiwa kupata kazi kwa mwajiri mmoja ambaye mkewe alikuwa ananilazimisha nilale na mumewe mara 3 kwa wiki,nilifanya kazi hiyo kwa mwka mmoja kwani nilihitaji pesa

Bahati sikuweza kupata ujauzito wake lakini namshukuru Mungu sikupata ugonjwa wowote ilhali siwezi tamani kufanya kazi ya nyumba tena kwa sababu ya mateso ambayo nilipokea

Lakini ukipata waajiri wazuri ni kazi nzuri na ambayo inawasaidia wasichana wengi."