Wavinya Ndeti alisoma digrii ya sayansi ya kompyuta kwa muda wa miezi 10

Muhtasari

•Barua iliyopakiwa na Wavinya ilifanya digrii ya sayansi ya kompyuta kutoka Septemba 1994 hadi Julai 1995, muda wa miezi 10 tu.

•Nchini Kenya, kozi ya shahada kwa kawaida huchukua angalau miaka minne, isipokuwa kwa kozi za uhandisi na matibabu ambazo huchukua miaka mitano na sita mtawalia

Mgombea ugavana wa Machakos Wavinya Ndeti akihutubia umma wakati wa mkutano wake wa kisiasa huko Athi River, eneo bunge la Mavoko Jumamosi, Aprili 2, 2022.
Mgombea ugavana wa Machakos Wavinya Ndeti akihutubia umma wakati wa mkutano wake wa kisiasa huko Athi River, eneo bunge la Mavoko Jumamosi, Aprili 2, 2022.
Image: MAKTABA

Mgombea Ugavana wa Machakos kwa tiketi ya Wiper Wavinya Ndeti Alhamisi alipakia barua kutoka Chuo Kikuu cha London South Bank kuthibitisha kuwa alihitimu pale.

Hatua hiyo hata hivyo haikumuendea vizuri  huku  maswali chungu nzima yakiibuliwa kuhusu uhalali wa shahada yake.

"Tunatumai kuwa hii itaondoa ipasavyo propaganda zisizo na msingi zinazoenezwa na washindani wetu na kuwanyamazisha wapiga domo," alisema kwenye chapisho la Facebook ambalo tayari ameshalifuta.

Barua iliyopakiwa na Wavinya ilifanya digrii ya sayansi ya kompyuta kutoka Septemba 1994 hadi Julai 1995, muda wa miezi 10 tu.

"Hii ni kuthibitisha kwamba mtu aliyetajwa hapo juu (Wavinya Oduwole) alikuwa mwanafunzi wa kutwa katika South Bank (sasa Chuo Kikuu cha London South Bank) kuanzia Septemba 1994 hadi Julai 1995 akisoma Kozi ya Masomo ya Kompyuta ya BSc (Hons)," Barua ya Chuo Kikuu cha London South Bank ya tarehe 15 Oktoba 2018 inasoma.

"Wavinya Oduwole alimaliza kozi hiyo kwa ufanisi na kutunukiwa Tuzo za Daraja la Chini la Pili (2.2) mnamo Julai 18 1995."

Taasisi hiyo, hata hivyo, haikuweza kutoa nakala za mitihani yak.

"Kwa bahati mbaya hatujaweza kutoa nakala kwa vile mfumo wetu wa rekodi za wanafunzi haukupata uwezo wa kuhifadhi taarifa zinazohitajika kwa nakala hadi Septemba 1998. Kabla ya tarehe hiyo, tuna rekodi ya uandikishaji, maendeleo na tuzo pekee," iliongeza barua.

Nchini Kenya, kozi ya shahada kwa kawaida huchukua angalau miaka minne, isipokuwa kwa kozi za uhandisi na matibabu ambazo huchukua miaka mitano na sita mtawalia.

Mgombea huyo wa ugavana hata hivyo ameshikilia kuwa shahada hiyo ni halali hata hivyo alionyesha imani kuwa atakuwa kwenye kura.

"Tunapigana bila kukatishwa tamaa na kero zao na kando. Lengo letu ni kushinda na kutoa kwa ajili ya wakazi wa Kaunti ya Machakos."

(Utafsiri: Samuel Maina)