Wachaneni na 'Sidechicks'- Uhuru awaambia wanaume walio kwenye ndoa

Muhtasari
  • Uhuru alijuta kwamba hati miliki katika baadhi ya familia zilisababisha mkanganyiko
  • "Anaenda benki kukopa pesa lakini anapotoka benki, anazitumia kwa wapenzi wake wa siri."
Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta amewataka wanaume kutumia pesa zao kwa busara kwa kutanguliza familia zao wala si wapenzi wa siri.

Akizungumza katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta siku ya Jumatano, Uhuru alisema baadhi ya wanaume wana tabia ya kutumia wakati mzuri na wapenzi wa siri na kuacha familia zao katika umaskini.

"Pesa ikiingia, akipitia mtaani anakutwa na kengine hapo. Anasahau yule aliwacha nyumbani, mali inaisha, unawacha familia na watoto wakifilisika… jameni wazee tubadilike..." alisema wakati akitoa hati miliki kwa sehemu ya Wakenya.

Uhuru alijuta kwamba hati miliki katika baadhi ya familia zilisababisha mkanganyiko.

Rais alisimulia jinsi wanaume wanavyotumia hatimiliki kama dhamana kukopa mikopo inayopotezwa kwa wapenzi wa siri badala ya kuinua familia nzima.

"Tatizo la kupata hati miliki ni kwamba mwanamume anapoipata, anahisi kuwa ni mali yake na hahitaji wengine," alisema.

"Anaenda benki kukopa pesa lakini anapotoka benki, anazitumia kwa wapenzi wake wa siri."

Uhuru aliwataka wanaume kurekebisha njia yao ya kufanya mambo na kutenda kwa kuwajibika kwa ajili ya maisha yao ya baadaye na ya watoto wao.

“Hati hii ni yako na familia yako. Unahitaji kuilinda ili familia yako ikukumbuke siku zijazo. Hebu tuchukulie hii kama hati muhimu tafadhali, "alisema.