Hisia za Miguna baada ya Diamond kutumbuiza Wakenya Kasarani

Mkutano wa Raila huko Kasarani umezua mijadala mikubwa kutoka kwa wapinzani katika kambi ya Kenya Kwanza.

Muhtasari
  • Kulingana na Miguna Miguna, ameangazia kuwa kambi ya Azimio haikuwa ya haki kwa Wakenya kwa sababu walimwalika Diamond Platnumz
Mgombea urais Raila Oinga na staa wa Bongo Diiamond Platnumz
Image: EZEKIEL AMING'A

Kinara wa ODM Raila Odinga alikuwa na wakati maalum wakati wa Mkutano Mkuu wa mwisho wa hadhara huko Kasarani kabla ya uchaguzi ujao siku ya Jumanne.

Wafuasi wa Azimio kutoka sehemu zote za nchi walifurika ukumbini.

Haya yanajiri wakati Naibu Rais William Ruto akiongoza kampeni ya fainali ya Kenya Kwanza katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo katika kinyang'anyiro cha kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.

Mkutano wa Raila huko Kasarani umezua mijadala mikubwa kutoka kwa wapinzani katika kambi ya Kenya Kwanza.

Haya yanajiri wakati ambapo mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz alipamba uwanja wa Kasarani kwa mkutano wa Azimio huku baadhi ya Wakenya wakiangazia kuwa mashabiki wengi walienda huko ili kumuona tu Diamond na wala si kwa malengo ya kisiasa.

Vivyo hivyo,  Miguna Miguna ametoa hisia kuhusu mkutano wa Raila Odinga huko Kasarani. Miguna ameshambulia kitendo cha Azimio kumwalika Diamond Platnumz kutumbuiza kwenye tamasha la Azimio Rally Kasarani.

Kulingana na Miguna Miguna, ameangazia kuwa kambi ya Azimio haikuwa ya haki kwa Wakenya kwa sababu walimwalika Diamond Platnumz.

Miguna anadai kuwa kambi ya Azimio haina uzalendo kwa kushindwa kuinua vipaji vya Wakenya hivyo wanamuziki wa Kenya wangetumbuiza na kulipwa badala ya kumwalika Diamond Platnumz.

"Kualika mwimbaji wa Kongo Mbilia Bel na msanii wa Tanzania Diamond kwenye mikutano ya kisiasa kulikusudiwa kuvutia vijana kwenye hafla hizo. Waliohudhuria sio wafuasi wa @RailaOdinga : Walienda huko kucheza na kutazama. Raila atapata 38% ya kura zote zilizopigwa

Walichagua kumwalika na kumlipa msanii wa Tanzania Diamond kwenye mkutano wao wa mwisho katika Uwanja wa Kasarani badala ya kumwinua mwanamuziki wa Kenya. Wasio na uzalendo."