Kuapishwa kwa Ruto kutaendelea bila wewe - Gachagua amwambia Uhuru

Alipata kura 7,176,141 dhidi ya 6,942,930 za Odinga.

Muhtasari
  • Hii, hata hivyo, itategemea matokeo ya ombi ambalo kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga anapanga kuwasilisha katika Mahakama ya Juu
RIGATHI GACHAGUA
Image: WLFRED NYANGARESI

Kuapishwa kwa rais mpya kutaendelea hata bila kuwepo kwa Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta, Naibu Rais Mteule Rigathi Gachagua amesema.

Hii, hata hivyo, itategemea matokeo ya ombi ambalo kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga anapanga kuwasilisha katika Mahakama ya Juu.

Mnamo Jumanne, Odinga aliapa kupinga kuchaguliwa kwa Naibu Rais William Ruto.

Alipata kura 7,176,141 dhidi ya 6,942,930 za Odinga.

Gachagua ambaye alikuwa akizungumza wakati wa mahojiano kwenye Kass TV alisema kutokuwepo kwake hakutaathiri kwa vyovyote mchakato wa mpito na makabidhiano.

Uhuru amekuwa kwenye rekodi akisema hatakabidhi mamlaka kwa Ruto.

Alitoa mfano wa kisa cha Marekani ambapo rais wa zamani Donald Trump ambaye alishindwa alitoa nafasi kubwa kwa hafla ya kuapishwa kwa kiongozi anayekuja Joe Biden.

“Kinachotakiwa tu wakati wa kuapishwa ni uwepo wa Jaji Mkuu, hata si upanga huo, hiyo ni sherehe tu,” alisema mbunge huyo wa Mathira anayemaliza muda wake.

Aliongeza:

"Lakini tunamwomba awe muungwana."