Majaji wa mahakama ya upeo wamenipa imani katika demokrasia yetu-Mutahi Ngunyi

Muhtasari
  • 'Vyovyote UAMUZI utakavyokuwa, siku ya pili ya kesi katika Mahakama ya Juu inanipa IMANI katika DEMOKRASIA yetu

Kufuatia kesi ya uchaguzi wa urais katika Mahakama ya Juu, Mutahi Ngunyi ameelezea imani yake katika utekelezaji wa demokrasia katika Mahakama ya upeo katika mchakato wa kusikilizwa kwa Malalamiko.

Kupitia kwenye ukurasa wa twitter alisema;

'Vyovyote UAMUZI utakavyokuwa, siku ya pili ya kesi katika Mahakama ya Juu inanipa IMANI katika DEMOKRASIA yetu. SI Wale mawakili, wakiwemo 'Toto' kwenye utetezi wa Ruto wanaonipa imani. Imani yangu kama Mwanasayansi wa Siasa inathibitishwa na MASWALI yaliyoulizwa na majaji."

Mahakama ya Juu leo ​​imefanya siku ya Pili ya kusikilizwa kwa kesi ya uchaguzi wa rais dhidi iliyowasilishwa na mpeperushaji bendera wa Azimio La Umoja One Kenya Alliance Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Karua wakipinga ushindi wa mteule wa urais William Samoei Ruto katika uchaguzi mkuu uliokamilika hivi majuzi.