(+video) Baya awasili bungeni kwa gari dogo "Nimechagua Vitz sababu mimi ni hustler"

Owen Baya alikitetea kiti chake eneo bunge la Kilifi North kupitia chama cha UDA

Muhtasari

• Owen Baya alikitetea kiti chake kwa tikiti ya UDA baada ya kujizolea kura 27,558 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Eliud Kalama wa ODM aliyejizolea kura 19699.

• Wabunge walikuwa wanaapishwa rasmi Alhamis kabla ya kushiriki chaguzi za kuwachagua spika na naibu wake.

Mbunge wa Kilifi North Owen Baya alichukua siku Alhamis wakati ambapo wabunge na maseneta waliochaguliwa katika uchaguzi wa Agosti 9 walikuwa wanawasili katika majengo ya bunge kula kiapo cha kuwatumikia wananchi kwa miaka 5 ijayo.

Baya ambaye awali alikuwa mbunge wa eneo hilo kwa tikiti ya chama cha ODM alikitetea kiti chake baada ya kuingia mrengo wa Ruto na kushindwa kwa chama cha UDA.

Wabunge mbali mbali waliwasili kwa magari makubwa yenye hadhi iliyotukuka ila ulipokuwa ni muda wa kuwasili kwa mbunge Baya, wengi waliokuwa katika lango la majengo ya bunge walishangaa kumuona akishuka kutoka kwa gari dogo aina ya Vitz.

Video moja ambayo imesambazwa inamuonesha Baya alizungumza na baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo la kushangaza kwani wengi hawakutarajia mwanasiasa mwenye hadhi yake tena mweney amehudumu bungeni kuwasili kwa gari lenye hadhi ya watu wenye kipato cha kadri kama hilo.

Baya alipoulizwa sababu yake ya kuamua kuteka anga kwa kuwasili kwa gari hilo, alisema kwamab yeye ni mpambanaji wa maisha ya chini, kwa kimombo wanaita ‘hustler’ -  kauli ambayo imekuwa ikitumiwa sana na wandani wa bosi wa chama cha UDA, William Ruto.

“Ninafika kwa staili yangu na gari dogo. Nimechagua hivi kwa sababu mimi ni mpambanaji wa chini (hustler) na tunakuja kwa njia ya kihasla. Tunaenda kuwachagua maspika, Moses Wetangula kama spika na Gladys Shollei kama naibu wake,” Owen Baya alizungumza kwa furaha kubwa.

Owen Baya alikitetea kiti chake kwa tikiti ya UDA baada ya kujizolea kura 27,558 dhidi ya wapinzani wake Eliud Kalama wa ODM aliyejizolea kura 19699, Ian Jefwa wa PAA aliyepata kura 4502, Elizabeth Ziro akajinyakulia kura 723 na Nobert Gongolo aliyepata 544.