Chuo kikuu cha Nairobi chawasherehekea Kingi na Wetangula "Ni wahitimu wetu"

Kingi na Wetangula walishinda viti vya maspika wa seneti na bunge la kitaifa mtawalia.

Muhtasari

• Wengine waliosherehekewa pia ni gavana wa Murang'a Irungu Kang'ata miongoni mwa mamia ya viongozi wengi waliohitimu kutoka chuo hicho akiwemo rais Ruto.

Maspika wa mabunge yote wapongezwa na chuo cha Nairobi
Spika Amason Kingi na Spika Moses Wetangula Maspika wa mabunge yote wapongezwa na chuo cha Nairobi
Image: MAKTABA

Chuo kikuu cha Niarobi ni moja ya vyuo vyenye jina kubwa barani Afrika na kinajulikana kwa kuwatoa viongozi katika nyadhifa mbali mbali nchini na nje ya nchi.

Chuo hicho sasa kwa mara nyingine kimechukulia Fahari kuteuliwa kwa maspika wa bunge la kitaifa na seneti pamoja na viongozi wengine walioteuliwa katika mchakato wa uchaguzi wa Agosti 9.

Katika ukurasa rasmi wa chuo hicho kweney Facebook, walichukua fursa hiyo ya kuwahongera maspika Moses Wetangula na Amason Kingi kama watu waliopitia mikononi mwa chuo hicho na kuwa viongozi wenye nguvu na ushawishi mkubwa katika siasa za nchini Kenya.

Pia picha ya tatu iliyopakiwa ni ya gavana wa sasa wa Murang’a, Irungu Kang’ata.

“Chuo Kikuu cha Nairobi ndicho zawadi inayoendelea kutoa! siku chache kabla ya kupokea kundi jipya la mwaka wa kwanza mnamo Septemba 19, 2022 na wiki moja baadaye kuachilia kikundi cha 67 cha wahitimu mnamo Septemba 23, 2022. Tunasimama ili kusherehekea wahitimu wetu ambao wanafanya mabadiliko katika nafasi walizomo. Hongera sana!!” Chuo cha Nairobi kilisema kweney Facebook.

Alhamis baada ya wabunge na maseneti kuapishwa, walishiriki mchakato wa kuwateua maspika na manaibu spika katika majumba yote mawili ya uongozi.

Katika bunge la kitaifa, aliyekuwa seneta wa Bungoma kabla ya kujiuzulu, Moses Wetangula aliteuliwa kama spika huku mwakilishi wa kike wa Uasin Gishu Gladys Boss Shollei akiteuliwa kama naibu spika.

Kwenye bunge la seneti, aliyekuwa gavana wa Kilifi Amason Kingi aliteuliwa kama spika huku Murungi Kathuri, seneta wa Meru akichukua wadhifa kama naibu spika.

Ilikuw ani siku ya kihistoria kwa muungano wa Kenya Kwanza ukiongozwa na rais mteule William Ruto baada ya kuramba nyadhifa hizo zote na hivyo kuzidisha ubabe wake katika mabunge yote.