Karibu kwa Ruto lakini hakuna kitu mtapata - Mbunge Osoro amwambia Ongwae na kundi lake

Karibu kwenye makazi rasmi ya Karen jiunge nasi ndio lakini lazima upange foleni. - Omanwa.

Muhtasari

• Gavana Ongwae aliopakia picha akisema pamoja na kundi la viongozi waliopoteza uchaguzi Kisii, walikutana na rais William Ruto. 

• Mbunge Sylvanus Osoro alisema hao walikuwa upinzani na hakuna kitu watapata kwani walienda kupigwa picha tu.

Mbunge Osoro awaambia Ongwae na kundi lake hakuna kitu watapata kwa Ruto
Mbunge Osoro awaambia Ongwae na kundi lake hakuna kitu watapata kwa Ruto
Image: Facebook

Jana, vuguvugu la viongozi walioondoka mamlakani katika kaunti ya Kisii walijumuika na rais mteule William Ruto katika makazi yake rami Karen Nairobi.

Gumzo kubwa liikuwa kwa sababu viongozi hao wote walikuwa ni wale waliokuwa mrengo wa upinzani Azimio la Umoja One Kenya wakiongozwa na gavana aliyemaliza kipindi chake cha miaka kumi James Ongwae, mwandani wa Raila Odinga pamoja na viongozi wengine walioangushwa katika uchaguzi wa Agosti 9 akiwemo aliyekuwa mwakilishi wa wanawake Janet Ong’era miongoni mwa wanasiasa wengine waliooneshwa kivumbi.

Waasi hao wa ODM kujiunga na kambi ya ushindi ya Ruto kulizua mjadala mkali haswa ikizingatiwa jinsi kundi hilo likiongozwa na Ongwae lilikuwa likimpigia debe Odinga na kupuuzilia mbali uwezekani wa Ruto kupata kura katika kaunti hiyo inayojulikana kuwa ngome ya Raila Odinga.

Gumzo hili lilikuja kutulizwa na mbunge wa Mugirango Kusini Sylavanus Osoro amabye ni rafiki wa karibu wa Ruto na ambaye alipitia mambo mengi mpaka kuibuka mshindi kwa chama cha UDA.

Osoro aliwatuliza watu wliokuwa wakiteta kwamab Ongwae na kundi lake wameenda kwa Ruto ili kujitafutia kazi. Alisema viongozi hao ambao walionekana kama wanajipendekeza upande wa serikali walienda huko lakini ni salamu tu waliruhusiwa na hakuna kitu kingine wanaweza pata.

“Tulia rafiki zangu, wale walikuja tu kupigwa picha. Wameenda. Tumewasamehe lakini hatuwezi sahau. Niamini mimi, hakuna kitu kingine kilizungumziwa na hakuna kitu kitakachozungumziwa. Sahau kabisa. Ni damu mpya ndio iko uongozini,” Osoro aliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook.

 Dennis Omanwa amabye pia ni rafiki wa Ruto alizungumzia suala hilo na kuwakaribisha Ongwae na kundi lake katika mrengo wa serikali ila akawatahadharisha kwamba hakuna kitu watapata lazima wapange foleni kwani hakuna kinachokuja kirahisi kama wanavyodhania.

“Karibu kwenye makazi rasmi ya Karen jiunge nasi ndio lakini lazima upange foleni. Hakuna njama ya mtu mkubwa hapa. Tutaondoka Karen hadi Ikulu Jumanne,” Omanwa alisindikiza maneno ya Osoro kwa kugongelea msumari wa mwisho.