Mwanafunzi wa chuo kikuu apatikana ameuawa ndani ya nyumba yake Ūthirū

Lucy Ngendo alisemekana kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi, mwaka wake wa 4

Muhtasari

• “Jumatano mchana, Ngendo, alipatikana ameuawa ndani ya nyumba yake kwenye vyumba vya studio huko Ūthirū

Lucy Ngendo mwanafunziwa chuo kikuu aliyepatikana ameuawa nyumbani kwake
Lucy Ngendo mwanafunziwa chuo kikuu aliyepatikana ameuawa nyumbani kwake
Image: Twitter

Wiki hii kumekuwa na picha za mwanadada mmoja anayesemekana kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi aliyeripotiwa kuuawa akiwa katika nyumba yake ya kulipia kodi viungaji mwa mji wa Nairobi.

Mwanadada huyo aliyetajwa kama Lucy Ngendo alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi kulingana na rafiki zake waliopakia kwenye Twitter wakililia haki na alikuwa katika mwaka wake wa nne.

Alikuwa anaishi katika makazi fulani eneo la Uthiru, mpakani mwa kaunti ya Kiambu na Nairobi na alipatikana ameuawa ndani ya  nyumba yake huku wandani wake wakibaki katika hali ya mshangao wasijue ni kwa nini aliuawa.

Mmoja kwa jina Yashpp aliyejitaja kama dadake mkubwa aliandika kwenye Twitter akiambatanisha picha zake za za makazi yale huku akitaka mtu yeyote anayeweza jua kilichojiri kuitaarifu familia ili haki kutendeka.

“Huyu ni dadangu mdogo, tafadhali kama kuna mtu yeyote anayeweza kuwa na habari kuhusu kilichojiri atutaarifu ili haki itendeke,” Yashpp aliandika huku akiretweet ujumbe wa mmoja Reke Maarie aliyetaja vyombo vya dola kulizamia tukio hilo ili kubaini wauaji na sababu zao za kufanya hivyo.

“Jumatano mchana, Ngendo, alipatikana ameuawa ndani ya nyumba yake kwenye vyumba vya studio huko Ūthirū. Inauma sana inapofika nyumbani. @NPSOfficial_KE @DCI_Kenya tafadhali fafanua jambo hili,” Reke Maarie aliandika.

“Tunaishi eneo moja na tumesikia tu jana usiku ... ni huzuni sana kilichompata. Roho yake iwe RIP na haki kwa familia yake” Mmoja aliyekuwa akiishi karibu na maeneo hayo kwa jina Njangiru alisikitika.

Baada ya wengi kutaja vyombo vya dola katika post hiyo, sasa inasubiriwa kuona idara za usalama ni hatua gani zitachukua ili kuhakikisha kwamba kitendawili cha mauaji hayo kimeteguliwa na familia ya Ngendo kupata haki.