Sisi hatukuwa watu wa kushinda, lakini Mungu ni nani? - rais Ruto

Ruto alisema kwamba waliambiwa hata wangeshinda hawangepewa ushindi kwani deepstate ingebatilisha kwa kupendelea mpinzani.

Muhtasari

• “Kwa mipango ya makadirio ya binadamu, sisi hatukuwa ni watu wa kushinda, lakini kwa sababu ya Mungu wa mbinguni jamani," - Ruto

Rais Ruto pamoja na viongozi wengine katika ibada ya kanisa Meru
Rais Ruto pamoja na viongozi wengine katika ibada ya kanisa Meru
Image: facebook

Rais mteule William Ruto Jumapili alikuwa katika kaunti ya Meru akiendeleza msururu wake wa kushiriki ibada za kutoa shukrani kutokana na ushindi wake kabla ya kuapishwa Septemba 13.

Ruto katika kanisa moja kaunti hiyo, alikimbuka jinsi alivyokuwa aandhalilishwa na baadhi ya viongozi waliounda serikali ya Jubilee pamoja kabla ya Handshake, pamoja pia na baadhi ya mawaziri na makatibu katika wizara waliokuwa wakimpiga vita vikali.

Kiongozi huyo wa UDA alisema kwamba licha ya hayo yote, lakini Mungu alisimama upande wake na kumhakikishia ushindi mpaka kuvunja baadhi yakile alikitaja kama tamaduni za siasa za Kenya kwamba hakuna naibu wa rais amewahi kuchaguliwa kwa mara ya kwanza na hakuna mwaansiasa amewahi jaribu bahati yake kuwania urais kwa mara ya kwanza na kushinda.

“Mambo ya binadamu wote yalikuwa kinyume na sisi, mnajua ya kwamba serikali tuliyounda waakti huo na upinzani waliungana kutupinga, makamishna, mawaziri, makatibu walikuwa wanatupinga. Hata tukaambiwa hakuna naibu wa rais ambaye amewahi kuchaguliwa kwa mara ya kwanza. alikumbuka kwa hisia kali Ruto.

"Tukaambiwa hakuna rais amechaguliwa akiwa amejaribu mara ya kwanza, hata tukaambiwa ikiwa tutashinda, hiyo kura hatutapewa kwa sababu deep state itaiba kura yetu, lakini Mungu akasimama na sisi” Ruto aliongeza.

Rais mteule wa tano alisema licha ya dhana zote hizo viongozi wa kanisa walisimama nao katika maombi na kupitia uwezo wa Mungu wakashinda na kuenda kinyume na mambo hayo yote.

“Kwa mipango ya makadirio ya binadamu, sisi hatukuwa ni watu wa kushinda, lakini kwa sababu ya Mungu wa mbinguni jamani, tuliwadhibitishia na kuwadhihirishia kuwa sivyo. Kama ingekuwa ni mipango ya binadamu, hatungeweza,” Ruto aliwaambia umati wa waumini.

Ruto anatarajiwa kuaishwa Jumanne Septemba 13 katika hafla ya kitaifa itakayofanyika uwanja wa Kasarani nairobi. atachukua hatamu kutoka kwa rais anayeondoka Uhuru Kenyatta kama rais wa tano wa Kenya tangu kujinyakulia uhuru kutoka kwa Wakoloni mwaka 1964.