Nakusihi uache kulia kwa ajili ya Wakenya - Wakili Donald kipkorir amshauri Raila

Usiangalie Kenya tena. Upendo wako haukustahili - Kipkorir

Muhtasari

• "Hatukustahili upendo na dhabihu yako. Wacha tuwe na mapungufu na minyororo yetu,” Kipkorir alimshauri Raila Odinga.

Kipkorir amemshauri Raila kutojihusisha na upinzani
Kipkorir amemshauri Raila kutojihusisha na upinzani
Image: Twitter, maktaba

Donald Kipkorir ni Mwansheria na mwandani wa kinara wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga kwa muda mrefu. Wiki jana alidokeza kwamab alianza kumuunga mkono Odinga tangia mwaka 2005.

Wakili huyo sasa amemtaka Odinga kutojihusisha na harakati za upinzani kabisa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kipkorir alisema kwamba kwa vile kesho uongozi mpya wa rais William Ruto unaanza rasmi, Raila hafai kujihusisha katika upinzani kuwatetea Wakenya kwani walimenga kwa kutompigia kura, kusababisha kuanguka katika jaribio lake la tano kuwania urais.

Kipkorir alimshauri Odinga kutowatetea Wakenya kama kiongozi wa upinzani na badala yake kujiweka mbali ili awaache Wakenya hao wateseka na upumbavu wao wakiwa katika minyororo.

“Mpendwa Raila Odinga, kesho unaanza Urais wa MHE William Ruto. Kutoka ndani ya moyo wangu, nakusihi uache kulia kwa ajili yetu. Usiangalie Kenya tena. Upendo wako haukustahili. Hatukustahili upendo na dhabihu yako. Wacha tuwe na mapungufu na minyororo yetu,” Kipkorir alimshauri Raila Odinga.

Watu wengi walionekana kukubaliana na ushauri huo kwa kusema kwamba kweli mzee Odinga amepigania nchi hii kwa njia nyingi muda mrefu ila Wakenya wenyewe hawaoni kama amejitoa kwao vya kutosha na kwa maana hiyo ni wakati sasa awaache wakaendeshwe kwa njia yoyote na serikali mpya pasi na kuwatetea kutoka upinzani.

“Tafadhali rafiki yangu mzuri hakikisha unamwambia Raila hili, sisi Wakenya hatuwezi kamwe kufahamu , ni chungu, mwache akae na kutazama mambo yanavyoendelea,” mtumizi wa Twitter kwa jina Shee alisema.