Sisi kushinda uchaguzi huu ni mkono wa Mungu, leo mtoto wa mtu kawaida amekuwa rais - Gachagua

Hatuchukui sifa kwa kushinda uchaguzi huu - Gachagua

Muhtasari

• Lazima niseme ukweli safari iliyo mbele yenu sio ya kufurahisha, naomba muendelee kumuombea rais na timu yake - Gachagua.

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta anatazama huku Naibu Rais Rigathi Gachagua akizungumzia vitisho na vitisho vya utawala uliopita alipokuwa akitoa hotuba yake ya kuapishwa katika uwanja wa Kasarani mnamo Septemba 13
Rais mstaafu Uhuru Kenyatta anatazama huku Naibu Rais Rigathi Gachagua akizungumzia vitisho na vitisho vya utawala uliopita alipokuwa akitoa hotuba yake ya kuapishwa katika uwanja wa Kasarani mnamo Septemba 13
Image: ANDREW KASUKU

Naibu rais Rigathi Gachaua katika hotuba yake ya kwanza kama naibu rais wa Kenya, alitema moto vikali kwa maneno ambayo yalionekana kumlenga rais anayeondoka rais Uhuru Kenyatta.

Gachagua alionekana kutupa kiazi moto kwenye mdomo wa Kenyatta kwa kile alisema kwamba akiwa rais aliwahangaisha sana wandani wa mrengo wa Kenya Kwanza unaoongozwa na rasi sasa William Ruto.

Mwanasiasa huyo mwenye misimamo mikali dhidi ya uongozi wa Kenyatta, alisema kwamba hata baada ya kuenda katika mifuko ya fedha, walipata hakuna pesa huko na kudai kwamba nchi italazimika kuanzia chini sana ili kuinuka.

Gachagua alisema kutokana na changamoto hizo, hakuna mtu hata mmoja aliyedhani Ruto angeshinda na hata ushindi huo hawawezi kusema ni wao bali ni uwezo wa Mungu.

“Hatuchukui sifa kwa kushinda uchaguzi huu. Haikuwezekana sisi kushinda uchaguzi huu. Ilikuwa ni kwa mkono wa Mungu kwamba leo, mtoto wa kawaida ameapishwa kama rais. Lazima niseme ukweli safari iliyo mbele yenu sio ya kufurahisha, naomba muendelee kumuombea rais na timu yake, tumerithi uchumi mbovu ambao unakaribia kukwama kiuchumi,” Gachagua aizungumza vikali huku rais Kenyatta akimtazama kwa mshangao mkubwa.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliyezungumza baadaye naye alionekana kuunga mkono matamshi ya Gachagua huku akisema kwamba changamoto kama hizo ambazo naibu rais alitaja ni kweli kwani wakati mmoja alitazama kipindi cha runinga moja ya humu nchini na kuhakikisha hayo maneno ya naibu rais.