(+video) Gachagua arudi gym kupiga tizi "Nataka kurudi shepu ya zamani nguo zinitoshee"

Sasa nataka kupunguza kutoka 94kg hadi 85kg - Gachagua

Muhtasari

• Gachagua alisema kwamba alizembea kufanay mazoezi kutokana na kuishi na wasi wasi wa kukwepa polisi ili asikamatwe.

• Aliahidi sasa kurudi katika mazoezi ili kurudisha shepu yake ya zamani.

Naibu rais ajaye Rigathi Gachagua asubuhi ya Jumanne akijiandaa kuhudhuria kuaoishwa kwake kama naibu rais wa pili chini ya katiba mpya ya mwaka 2010, alionekana akiwa anafanya mazoezi katika gym moja huko Karena Nairobi.

Gachagua ambaye kabla ya kuchaguliwa kuwa naibu rais alikuwa mbunge wa Mathira huko Nyeri alizungumzia suala hilo na kusema kwamba hii si mara yake ya kwanza kushiriki mazoezi kweney gym bali ilikuwa ni mazoea yake.

Alisema ilibidi amesitisha kwa takribani miaka 4 iliyopita kwa kile alisema kwamba simu yake ilikuwa imemulikwa na watu waliokuwa wakifuatilia mienendo yake pamoja na familia yake.

“Haya yalikuwa ni mazoea yangu miaka 4-5 iliyopita ndio niliweka hii gyma hapa kwa ajili ya mazoezi. Lakini katika miaka michache iliyopita sikuweza kuja huku kwa sababu nilikuwa na waswasi wa jinsi nitakavyoishi ili nisiuawe. Unajua jinsi ya kukwepa maafisa wa polisi, jinsi ya kutafuta chakula,” Gachagua alisema.

Mwanasiasa huyo alisema kwamab katika kipindi hicho ndio alijipata mwili wake umekua katika shepu na muonekano mbaya kutokana na kuzembea kufanay mazoezi.

Alizingumzia pia wale wanaokejeli mavazi yake kuwa ni makubwa kumzidi na kusema hao hawajui kile amabcho amekipitia. Alidokeza sasa Kwenda mbele anataka kupunguza uzito wa kilo za mwili kutoka 94 hadi 85 ili kurudi katika hali yake ya zamani nguo kumtoshea na kuboresha muonekano.

“Nilipata uzito mwingi wakati huo. Sasa nataka kupunguza kutoka 94kg hadi 85kg, kuwa na umbo na kutoshea nguo zangu kuukuu. Watu wanapozungumza kuhusu mtindo na mwonekano wangu, mimi hucheka tu. Hawajui ninatoka wapi. Nilianzisha gym hii miaka 15 iliyopita, lakini kwa miaka minne na nusu iliyopita, sijaweza kufanya mazoezi. Lakini sasa nitakuja hapa,” Gachagua alisema.