"Wakati wa boychild" Mama Dorcas Gachagua aapa kupa kipaumbele suala la mtoto wa kiume

Dorcas ni mama wa watoto wawili wa kiume

Muhtasari

• Ukizunguka utaona tu jinsi mtoto wa kiume ametengwa mijini wengi wanatumia dawa za kulevya

mama Dorcas Gachagua amesema yeye atawapa watoto wa kiume kipaumbele zaidi
mama Dorcas Gachagua amesema yeye atawapa watoto wa kiume kipaumbele zaidi
Image: Maktaba

Mama wa pili wa taifa ajaye Dorcas Gachagua kwa mara ya kwanza tangu kuanza kugonga vichwa vya habari amezungumzia umaarufu huo ambao ameupata tangu mumewe Rigathi Gachagua na William Ruto kushinda uchaguzi kama rais na naibu wake mtawalia.

Alisema kwamab siku hizi huwa anawekewa usalama mwingi sana tangu kutangazwa kinyume na alivyokuwa amezoea maisha yake ya awali, hata hana ule uhuru wa kuenda kufanay ununuzi katika maduka ya jumla kama alivyokuwa akifanay awali.

Dorcas alifichua kwamba amekuwa rais kwa zaidi ya miaka 11 na siku hizi hata kama bado anahudumu kama mchungaji lakini amekuwa akipewa ulinzi.

Dorcas alisema kwamba katika nafasi yake kama mama taifa wa pili, yeye atalifanyia kazi suala na kupigania haki za mtoto wa kiume, haswa ikizingatiwa kwamab yeye ni mama wa vijana wa kiume wawili.

“Mimi nitalipa kipaumbele suala la mtoto wa kiume na pia wale watu waliotengwa katika jamii. Nina wakfu wa kutoa msaada kote nchini na kwa wajane. Nadhani kama utazunguka hata hauitaji kuuliza mbona mtoto wa kiume, ukizunguka utaona tu jinsi mtoto wa kiume ametengwa mijini wengi wanatumia dawa za kulevya wakiwa katika hali ya unyongovu na kutengwa. Ningependa kuona watoto wote kiume na kike wamelelewa katika mazingira yanayowakubali wote ili kuwakwamua” Dorcas alisema.

Alisema kwamba katika ofisi yake atakuwa anafanya kazi kama msaidizi wa naibu rais na ndio atalisukuma suala la kupigania mtoto wa kiume.

Alisema ana watoto wawili wa kiume, mmoja akiwa ni daktari na mwingine akifanya kazi kweney benki kama mtaalamu wa masuala ya kompyuta na mifumo ya kidijitali.