Mwanaume amuua ndugu yake kwa mzozo wa nyama matumbo ya Ksh 50

Mwanaume huyo alinunua nyama yake na kuiweka kwenye ua kabla ya kuenda haja ndogo, aliporudi alipata nyama yake haiko

Muhtasari

• Polisi walisema mtuhumiwa alimkata ndugu yake kichwani kwa panga katika kijiji cha Ihumbu kwa kumtuhumu kwamba ameiba nyama yake.

Nyama Chom kwa viazi
Image: BBC

Polisi katika kaunti ya Murang'a wanamsaka mwanamume mmoja wa miaka 30 anayeshukiwa kumuua kaka yake mkubwa kwa kukosa nyama aina ya matumbo yenye thamani ya KSh 50.

Katikac tukio hilo lililoripotiwa kutokea wikendi iliyopita, gazeti la Nation linasema kwamba kaka huyo alipata nyama yake aliyoinunua kwa thamani ya shilingi hamsini imetoweka kwa njia isiyojulikana ambapo alimshuku ndugu yake na huo ndio ulikuwa mwanzo wa zogo baina yao.

Polisi walisema mtuhumiwa alimkata ndugu yake kichwani kwa panga katika kijiji cha Ihumbu. Baba yao, Bw Onesmus Nduati, alisema alisikia zogo katika boma lake na kukimbia alipata wawili hao wakizozana.

“Mkubwa mmoja alikuwa anasema kaka yake amemuibia kifurushi cha matumbo, mshitakiwa alikana, mdogo alikuwa na panga mkononi... nilijaribu kuwasihi waache ugomvi na badala yake tulizungumzie suala hilo," Bwana Nduati alisema kulingana na gazeti la Nation.

Marehemu alikuwa amenunua nyama yake na kuiwekelea katika ua moja huku akienda haja ndogo na aliporudi alipata nyama yake haipo. Hapo ndipo alitafakari kwamba kwa vile ndugu yake alikuwa nyumbani basi ndiye huendqa alivizia nyama yake na kuichukua.

Baba yao alisema mtoto mdogo, "ambaye kwa ujumla ni mgomvi na mwenye hasira kali kama Mt Everest, hakutaka kusuluhisha mzozo huo kwa amani lakini alimshambulia kaka yake mwenye umri wa miaka 36 kwa panga".