Marekani: Rais Ruto akutana na Cosmo Choy, mtetezi mkali wa sera zake

Cosmo Choy ni mmoja wa Wakenya wanaoishi ughaibuni na ambao walikuwa waanfuatilia siasa za humu nchini kwa ukaribu mno.

Muhtasari

• “Moja kwa moja na rais wa tano William Ruto,” Cosmo Choy aliandika.

Cosmo Choy hatimaye akutana na Ruto Marekani
Cosmo Choy hatimaye akutana na Ruto Marekani
Image: twitter

Cosmo Choy, mtetezi mkubwa wa sera za rais William Ruto enzi za kampeni zake hatimaye amekutana na rais huyo nchini Marekani.

Wengi walimjua Cosmo Choy kutokana na kauli zake akiwasuta wale waliokuwa wakimpinga Ruto kipindi hicho akiwa kama naibu rais.

Cosmo Choy aligonga vichwa vya habari nchini Kenya baada ta klipu fulani yenye ukakasi kuibuliwa akimkejeli rais Uhuru Kenyatta pamoja na familia yake haswa mama wa kwanza wa taifa, Ngina Kenyatta,

Ngina Kenyatta alitukanwa vibaya mno na mwanaume huyo kwa kile alijitokeza kuwarai Wakenya katika hafla moja ya mazishi kutaka wafuate mwelekeo wa kisiasa wa mwanawe, Uhuru Kenyatta.

Kenyatta alikuwa anampigia debe kinara wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga baada ya kumgeuka naibu wake William Ruto.

Cosmo Choy, Mkenya anaishi na kujishughulisha kutafuta riziki nchini Marekani alifanya msururu wa klipu akimtetea Ruto dhidi ya mamia ya wanasiasa waliokuwa wakimpinga na kukejeli manifesto yake ya Bottoms Up.

Baada ya kukutana na Ruto nchini Marekani, Cosmo Choy aliandika kwenye Twitter yake na kupakia picha kwamba hatimaye amekutana naye moja kwa moja.

“Moja kwa moja na rais wa tano William Ruto,” Cosmo Choy aliandika.

Rais Ruto yuko Marekani kwa ziara ya juma moja kuhudhuria kongamano la baraza la umoja wa mataifa, linalofanyika kwa mara ya 77.

Ruto aliongozana na viongozi wengine Kwenda Marekani baada ya kumaliza kuhudhuria msiba wa aliyekuwa malkia wa Uingereza, Elizabeth wa pili huko London.