(+video) Polisi wafurahisha katika klipu ya wimbo wa 'Vaida'

Vaida ni wimbo ambao umefanywa na mwanamuziki wa injili Harry Richie

Muhtasari

• "Chochote unachofanya, tunafanya vizuri zaidi," NPS waliandika kwenye Twitter.

Tume ya kitaifa ya hudumu kwa polisi NPS imepakia video ya polisi wakifanya klipu ya wimbo wa Kiluhya ambao unazidi kurindima maeneo yote nchini, Vaida wake msanii Harry Richy.

Katika video hiyo, NPS walijipiga kifua na kutamba kwamba hata wao pia wanaweza kushiriki katika mambo yanayotrend nchini kwa ufasaha, kumaliza dhana ambayo imekuwa kwa muda mrefu katika vichwa vya rais kwamba polisi si binadamu wa kawaida.

Ilianza na utangulizi wa wimbo wa Vaida kabla ya afia mmoja wa polisi kuonekana aizicharaza ngoma kwa mikono yake na wenzake wakizikwenda kwa ala mbali mbali za muziki huo.

Walipokuwa wanafurahia kurindima sauti mbalimbali kwa ala, afisa mmoja wa kiume anacheza dansi katikati ya wanaume waliovalia sare waliokuwa wameunda duara. Kisha video hiyo ilionyesha askari wa kike ambaye aliwashangaza watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa mchezo mzuri wa bega huku akionyesha jinsi ngoma hiyo inapaswa kufanywa.

Alitikisa mabega yake na, wakati fulani, akampa mwenzake simu yake huku akiendelea kuwavutia watu na ngoma yake huku akifanya kuzunguka kama pia.

 "Densi ya "Vaida". Jinsi tunavyoifanya hata sisi tukiwa kwenye sare za polisi. Chochote unachofanya, tunafanya vizuri zaidi," NPS waliandika kwenye Twitter.

Wengi walifurahishwa na unenguaji wa mabega wa mama polisi huyo ambako walisema haikosi atakuwa ana chembe chembe za damu kutoka upande wa magharibi mwa Kenya.

Wimbo wa Vaida umewafurahisha wengi ambapo mpaka sasa watu mashuhuri mbali mbali wamejitoma mduarani kunengua kwa furaha kwa wimbo huo.

Mwanatiktoker Azziad alikuwa wa kwanza kufanya klipu hiyo iliyoshabikiwa pakubwa na kisha wengine pia walifuata mkondo akiwemo mwigizaji Nyaboke Moraa miongoni mwa wengine.