(+video) Vijana wabunifu wameniita Riggy G, Sidhani kama ni jina baya - DP Gachagua

Gachagua alikuwa akizungumza katika hafla ya miziki ya shule nchini Kenya iliyofanyika Kisumu.

Muhtasari

• Na sidhani kama ni jina baya, eeh” Gachagua alizungumza huku watu wakijawa na bashasha.

Naibu rais Rigathi Gachagua hatimaye amekubali jina la kimajazi alilobandikwa na baadhi ya Wakenya mitandaoni.

Jina Riggy G ambalo lilianzia ukurasa wa Tweeter linasemekana kuwa ufupisho wa jina lake Rigathi Gachagua na wengi wamekuwa wakimwita jina hilo haswa katika mitandao ya kijamii.

Katika klipu moja ambayo imepakiwa mitandaoni, inaonesha Rigathi Gachagua akizungumza kwenye hafla ya miziki ya shule nchini Kenya iliyoandaliwa Kisumu na ambapo pamoja na viongozi wengine walihudhuria Ijumaa.

Gachagua alisema kwamba jina hilo linaonesha jinsi vijana wa Kenya ni wabunifu kwa njia ya kipekee na kulikubali kwamba haoni ni baya kwa sababu lina mirindimo ya nyuzi zenye ladha ya aina yake.

“Nimeshangazwa kwamba vijana wetu wadogo wamenipatia jina la kimajazi. Wameangalia katika majina yangu mawili, Rigathi Gachagua, wakatafuta kitu ambacho kitakuwa rahisi kutamkika, rahisi kusikika kwa mrindimo mzuri na kuniita Riggy G. Na sidhani kama ni jina baya, eeh” Gachagua alizungumza huku watu wakijawa na bashasha.

Gachagua pia alitoaahadi mbali mbali akiwa jijini Kisumu kama vile kusimamia masomo ya binti mmoja aliyeimba wimbo kwa sauti iliyuomfurahisha naibu wa rais.

Binti huyo ambaye ana ulemavu wa macho ni mwanafunzi katika shule ya vipofu ya Thika na Gachagua aliahidi kumsimamia katika masomo yake mpaka kileleni, taarifa ambayo wengi wameishabikia kwenye mitandao ya kijamii. Haya basi sasa ni rasmi naibu rais wa Kenya ni Riggy G!