Video yaibuliwa jinsi Ruto alikuwa akifanya mazoezi ya hotuba za kampeni zake

Video hiyo ilivujishwa na Dennis Itumbi akisema kwamba Ruto hakuwa anakurupuka tu na kuenda kampeni kuzungumza na watu bai ni kitu alikuwa amejiandaa vilivyo.

Muhtasari

• "Kuzingatia. Kujitolea. Kujituma na kujitoa wakati kwa wote..” Itumbi aliandika.

Msemaji wa Hustler Nation, kipengee cha kampeni za William Ruto, Dennis itumbi amefichua kwamba mgombea urais wao ambaye sasa ni rais William Ruto hakulala na kuamka tu kujipta akiwa rais.

Itumbi alipakia klipu ya video akisema kwamba Ruto alikuwa anatia bidii katika kujitayarisha kwa baadhio ya jumbe na maneno ambayo angezungumza na umma wakati wa kampeni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Itumbi alipakia klipu hjiyo ikimuonesha Dkt. Ruto akiwa anajiaandaa kusoma jumbe hizo mbele ya kamera.

Kitu ambacho Itumbi alisema kiliwasaidia kama Kenya Kwanza kujipanga vizuri kabla ya kuondoka kwenda nyanjani kunadi sera zao kwa wananchi.

“Baada ya Mjadala wa Urais, Mgombea Urais wa Kenya Kwanza wakati huo, William Ruto, alichukua saa tatu kurekodi jumbe za Mawasiliano ya Umma. Hapa angalia kwenye Dry Run, kabla ya kurekodi halisi... Kuzingatia. Kujitolea. Kujituma na kujitoa wakati kwa wote..” Itumbi aliandika.

Wiki jana, Itumbi pia kupitia ukurasa wake wa Twitter alipakia picha akionesha jinsi naibu rais Rigathi Gachagua kipindi hicho akiwa kama mgombea mwenza wa Ruto alijiandaa kuelekea mdahalo wa manaibu wagombea urais.

Itumbi alieleza kwamba hata iliwabidi wamtafute mwanamke ambaye angechukua nafasi ya aliyekuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga Martha Karua ambaye walisema ni mtu kazi yake ingekuwa kumchukiza ili kuona jinsi atakavyofanya katika siku yenyewe ya ndovu kumla mwanawe.

Na hakika, Gachagua aling’ara kweli kweli kwenye mdahalo ule wa wagombea wenza huku Karua akishindwa kufana kama ambavyo wengi walikuwa wametegemea.Baada ya juhudi hizi zote za kujituma, Ruto aliingia katika vitabu vya historia kuwa naibu wa rais wa kwanza tangu uhuru wa Kenya kuwahi kuwania urais na kushinda.

Pia rais Ruto alivunja rekodi ya kuwa Mkenya wa kwanza kujaribu bahati yake katika urais na kushinda kwa mara ya kwanza.Ruto alipata kura zaidi ya milioni 7.1 na kushinda urais.

Alikuwa akikabiliana na Raila Odinga, mpinzani wake mkuu ambaye zaidi ya Wakenya milioni 6.9 walimpigia kura.