Huyu polisi alikuwa alikuwa afunge ndoa Desemba, sasa hayuko! - Afisa Sammy Ngare

Ngare alichukizwa na jinsi polisi wanavyothaminiwa licha ya kujitolea katika kulinda usalama.

Muhtasari

• Ni kwa Neema ya Mungu tu tunarudi nyumbani tukiwa hai..yote kwa yote Mungu hatatuacha kamwe - Ngare.

Afisa Ngare amemuomboleza afisa wa polisi mwenzake aliyeuawa Turkana
Afisa Ngare amemuomboleza afisa wa polisi mwenzake aliyeuawa Turkana
Image: Facebook

Afisa maarufu wa polisi nchini Kenya Sammy Ondimu Ngare amewaomboleza maafisa wa polisi waliopoteza maisha yao katika shambulio la wezi wa mifugo wikendi iliyopita huko Turkana.

Ondimu ambaye ni maarufu kutokana na wakfu wake wa kufanya kazi kwa za kutia moyo kwenye jamii alionesha kutoridhishwa kwake na jinsi maafisa wa polisi wanavyochukuliwa hali ya kuwa wao ndio hujitoa hadi tone la mwisho la damu kuwahudumia wananchi haswa nyakati za kutishia usalama.

“Jana tulipoteza Askari Polisi 8 na Wakenya wengine watatu pekee kwenye vyombo vya habari na hakukuwa na taarifa za hivi punde kwenye vyombo vya habari..lakini wakati kuhusu raia wa kawaida tunachangia damu na pesa taslimu pamoja na siku 2 za kuomboleza kwa heshima na bendera nusu mlingoti....Kwani Askari sio watoto wa watu???? Moyo wangu unavuja damu jameni.. Kwanini kwanini??” Ngare aliandika kwenye Facebook yake.

Ngare alifuatisha picha ya polisi mmoja aliyeuawa ujumbe huo mrefu wenye hisia za kutia huruma na kusema kwamba hata wao pia licha ya kujitoa kuhakikisha usalama wa rais, lakini wanahitaji kuthaminiwa sababu pia wana familia zinazowategemea, watoto wanaowaita baba na majukumu mengine kama Wakenya wazalendo.

“Inaumiza sana wakati baadhi yetu tunajitoa katika maisha yetu kuwahudumia watu wengine, Wakenya. Kukosa usingizi usiku...miezi bila kuona wapendwa wetu(familia)...Sisi pia tunahitaji kusikia watoto wetu wakituita baba au mama, tunazungumza kwa simu tu ...lakini tunajitolea haya yote ili wewe na watoto wako mufurahie maisha..tunapokufa tukiwa katika majukumu hakuna anayeona.. familia zimeachwa bila baba zao...” Ngare alizidi kutema maneno kwa hisia.

Alimuomboleza afisa mmoja kati ya hao kuwa ni kijana mdogo ambaye sasa ndoto yake ya kuanzisha familia Desemba hii imefutiliwa mbali na kutokomezwa kabisa asiwahi sikika wala kuonana tena.

“Jamaa kwenye picha hapa chini alikuwa miongoni mwa maafisa wa GSU waliopoteza maisha yao pale Turkana.. Afisa kijana mahiri kutoka eneo la nyumbani kwangu Kisii...Afisa ambaye alikuwa karibu kuanzisha familia Desemba hii..Ooh Mungu! Hayupo tena…Ni kwa Neema ya Mungu tu tunarudi nyumbani tukiwa hai..yote kwa yote Mungu hatatuacha kamwe....Mungu anatutazama Kila Siku..” Ngare aliuomboleza afisa huyo marehemu sasa.