'Nina wasiwasi kuhusu mahakama ya Kenya'Seneta Ledama Olekina adai

"Nina wasiwasi kuhusu Mahakama ya Kenya! Hivi karibuni simu Nyekundu ambayo Mutunga alisema haikuwahi kuita inaweza kuanza kuita".

Muhtasari
  • Mnamo Agosti 15 mahakama kuu ilimtangaza William Ruto kuwa rais wa tano wa jamuhuri ya Kenya

Seneta wa Narok H.E Ledama Olekina amedokeza kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter akidai kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusu mahakama ya Kenya.

Kulingana naye aliyekuwa Jaji Mkuu wa zamani Mutunga alisema kuwa wakati wake simu yao haikuweza kuita hivi karibuni.

"Nina wasiwasi kuhusu Mahakama ya Kenya! Hivi karibuni simu Nyekundu ambayo Mutunga alisema haikuwahi kuita inaweza kuanza kuita". Seneta Ledama Olekina alisema.

Baadhi ya viongozi wa Muungano wa Muungano wa Azimio One Kenya Alliance wameendelea kulalamikia mahakama ya Kenya baada ya Azimio kushindwa katika ombi la urais katika mahakama kuu.

Mnamo Agosti 15 mahakama kuu ilimtangaza William Ruto kuwa rais wa tano wa jamuhuri ya Kenya.