(+video) DP Gachagua: Nitazidi kumkumbusha rais Ruto kuhusu mkataba na makanisa

Nilichukua Biblia na kuapa kumsaidia rais Ruto - achagua alisema

Muhtasari

• Gachagua alisema kwamba kazi yake kuwa ni kumsaidia rais Ruto na ataizidi kuifanya kazi hiyo kumkumbusha.

Naibu rais Rigathi Gachagua amedhibitisha kwamba rais William Ruto aliweka mikataba na watu wa kanisa na atazidi kumkumbusha rais.

Akizungumza katika ibada iliyandaliwa Jumapili katika ikulu ya Nairobi, Gachagua alisema kwamba anajua fika jukumu lake ni kumsaidia rais na katika hilo akaahidi kuendelea kumsaidia kutosahau ahadi zake kwa kanisa.

“Nilichukua Biblia na kuapa kumsaidia, kwa niaba yenu, nitaendelea kumkumbusha kwenye MOU yetu pamoja na nyinyi, kuhusu masuala ya kanisa, hata kama ana majukumu mengine mengi, ni wajibu wangu kumkumbusha," Gachagua alisema.

Matamshi haya ya Gachagua yanakuja siku moja tu baada ya minong’ono mikali kuibuliwa kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mkataba baina ya serikali ya Ruto na makanisa nchini Kenya.

Itakumbukwa Jumamosi jarida la Nation lilifanya taarifa kuzungumzia suala hilo la mkataba baina ya makanisa na serikali ya Ruto.

Askofu Samuel Njiriri wa Shirikisho la Makanisa ya Wainjilisti na Wakristo Wenyeji Kenya alinukuliwa na jarida hilo akidhibitisha kuwa Ruto alisaini mkataba na makanisa, mkataba ambao uliwashawishi watu wa kanisa kujibwaga nyuma yake na kumpigia kura kwa wingi.

Kulingana na taarifa hiyo, Masuala katika mkataba huo ni pamoja na mgao wa bajeti kwa wachungaji, fedha za serikali zisizo na viwango sifuri kuwezesha shughuli za kanisa kupitia Sacco ya makasisi, ugawaji wa ardhi kwa makanisa, na uteuzi wa tume, mashirika ya serikali, misheni za kigeni na Baraza la Mawaziri Wanataka uhuru wa makanisa yaliyohakikishwa kwa kuondoa kusitishwa kwa usajili, kuanzisha ofisi ya msajili wa mashirika ya kidini na kuunda hati ya Baraza la Mawaziri kwa masuala ya kidini.