Makondakta waliorekodiwa wakifanya sarakasi kwenye basi wakamatwa

Huduma ya polisi ya kitaifa watangaza kuwa wamewakamata makondakta waliokuwa wakibembea na kufanya sarakasi kwa mlango wa gari

Muhtasari

• Waliwashauri matatu nyingine na magari mengine ya kusafirisha abiria kuwa na utulivu na kuwa na nidhamu kama huo ili kupata heshima na sifa njema miongoni mwa abiria.

Polisi wamesema kuwa wawili hao wamekamatwa.
Makondakta wawili wafanya sarakasi kwenye basi Nairobi. Polisi wamesema kuwa wawili hao wamekamatwa.
Image: HISANI

Polisi wamewakamata makondakta wawili waliokuwa wakidandia basi na kufanya sarakasi kwenye mlango katika barabara moja jijini Nairobi.

Dereva wa gari hilo pia alikamatwa baada ya video kuenezwa mitandaoni na kuwafikia maafisa ambao waliwatia mbaroni kwa kukiuka sheria za trafiki.

Kitengo cha Huduma kwa polisi kilisema kuwa sarakasi walizokuwa wakifanya makondakta hao zilihatarisha maisha yao,

"Huduma ya polisi ya kitaifa inakemea tabia hatari na za kiholela ulioweka maisha ya watu waliokuwa kwenye gari hilo na watumizi wa barabara hatarini. Tabia hiyo inaonyesha kutowajibika wa watu hawa na hatutasamehe tabia kama hii barabarani," NPS ilisema.

Waliwaonya watu wenye tabia kama za kukiuka sheria za barabarani kuwa yeyote watatiwa mbaroni watakapopatikana. 

Huduma hiyo pia ilipongeza sacco zilizo na heshima barabarani na kuwa na usawa na utulivu barabarani.

Huduma hiyo ilishauri sacco nyingine za magari kukemea tabia kama hiyo iliyoonyeshwa kwenye video hiyo. Wasimamizi waliagizwa wasikubali watu waliokosa nidhamu kwenye magari yao.

"NPS na NTSA bado inachunguza mienendo barabarani ili kuhakikisha hakuna ukiukaji wa sheria za barabarani na kuwa zimeheshimiwa na kila mtu," Taarifa ilisoma.