Maoni kinzani baada ya jamaa kuonekana na jeneza sebuleni, asema ni la kuhifadhi nguo

Jamaa huyo ambaye hakutambulika kwa jina alionekana amejilaza kwenye kiti ndani mwake na mbele yake kuna jeneza.

Muhtasari

• Baadhi ya wanamitandaoni walimshuku kuwa huenda anajihusisha na masuala ya ushirikina.

Image: Tweeter

Mtumiaji wa Twitter amezua gumzo baada ya Wanamtandao kuona jeneza ndani ya nyumba yake.

Katika tukio hilo lisolo la kawaida, picha ya sebule ya jamaa huyo ambaye bado hajatambulika ni nani ilisambazwa kweney mtandao wa Tweeter ikimuonesha akiwa ametebwereka juu ya kochi lake huku mbele yako kuna jeneza lililowekwa chini sakafuni kwenye kona moja ya nyumba yake.

Baadhi ya watu waliosambaza picha hiyo kwenye Tweeter walisema kuwa jamaa huyo alikuwa amechapisha picha inayoonyesha mambo ya ndani ya nyumba yake, na alipoulizwa kwa nini anaweka jeneza ndani ya nyumba hiyo, alidai kuwa analitumia kuhifadhi nguo zake.

Picha imesambaa tangu wakati huo na kuvutia maoni mengi kutoka kwa Wanamtandao huku baadhi ya watu wakimshuku kuwa huenda anajihusisha na mambo ya ushirikina.

Picha hiyo inaonesha sebule ya kawaida tu iliyopo na kochi la kuketi watu watatu ambako ndio jamaa huyo ameketi kwa kujinyoosha miguu juu ya kochi zima na mbele yake kuna meza na kiti cha plastiki, kwa mbali pia kochi lingine linaonekana na kando yake sasa ndio jeneza limejinafasi sakafuni.

Juu ya jeneza hilo kulionekana mishumaa na pambo la msalaba, jambo ambalo lilivutia maoni kinzani kutoka kwa baadhi ya wanamitandao haswa baada ya uvumi kuzuka kuwa jeneza hilo linatumika na jamaa mhusika kama hifadhi ya nguo.

“Ni kama sanduku lingine lolote lililotengenezwa kwa mbao.😅 Ninahitaji vile ili kuwaepusha wageni katika kipindi hiki kigumu cha kiuchumi. Huyo ni genious” mmoja kwa jina Maina Janet aliandika.

“Hatimaye mauti yatamkuta, atayakosa na atabadilisha nguo,” Monica Waliaula alisema.